Mbunge wa Kigoma Mjini na msanii Clayton Chipando, maarufu kama Baba Levo, ameomba radhi kufuatia mvutano uliotokea kati yake na afisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), katika sakata lililohusisha gari la mwanamuziki Ommy Dimpoz.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Baba Levo amesema amefikia hatua hiyo baada ya kutambua kuwa huenda baadhi ya watu bado wana kinyongo kutokana na yaliyotokea, akisema, “Pamoja na yote niliyoongea, lakini inawezekana bado kuna watu wana kinyongo kwenye hili jambo lililotokea kati yangu na afisa wa TRA. Naomba radhi pale nilipokosea.”
Mvutano huo uliibua mjadala kwenye mitandao ya kijamii, baada ya video za mabishano kati ya Baba Levo na afisa huyo wa TRA kusambaa, huku sakata hilo likihusisha utekelezaji wa majukumu ya mamlaka hiyo kuhusu gari la Ommy Dimpoz.
