Maganga Wa Kienyeji Abaka Mteja Wake Mtwara

Baba Abby
0

 

Uganga

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara linamshikilia Shafii Rashid (23), mganga wa kienyeji na mkazi wa Kijiji cha Nanguruwe, Wilaya ya Mtwara, kwa tuhuma za kumbaka mwanamke mwenye umri wa miaka 30 ambaye alikuwa mteja wake.


Kwa mujibu wa Polisi, tukio hilo linadaiwa kutokea Septemba 14, 2026, nyumbani kwa mwanamke huyo katika Kata ya Ziwani, baada ya mtuhumiwa kudaiwa kumlaghai kuwa anampaka dawa ambayo ingesaidia kutatua changamoto iliyokuwa ikimsumbua mtoto wake.


Polisi inaendelea na uchunguzi wa tukio hilo, huku mtuhumiwa akitarajiwa kufikishwa mahakamani baada ya uchunguzi.

Tags

Post a Comment

0 Comments

Post a Comment (0)

#buttons=(Ok, Go it!) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Check Now
Ok, Go it!