Sintofahamu kuhusu mahali alipo aliyekuwa Makamu wa Rais wa Tanzania, Dkt. Emmanuel Nchimbi, imeendelea, tangu alipotangaza kujiuzulu wadhifa huo Agosti 25, 2026.
Mjadala huo umechochewa zaidi na kauli ya Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa, Ally Hapi, ambaye alipoulizwa alipo Dkt. Nchimbi alisema suala hilo linapaswa kuulizwa familia yake.
Wakati huo huo, Katibu Mkuu wa ACT-Wazalendo, Ado Shaibu, ameitaka familia ya Dkt. Nchimbi na vyombo vya dola kutoa ufafanuzi kuhusu usalama na hali yake, ili kuondoa sintofahamu inayoendelea.
Hadi sasa, taarifa rasmi kuhusu alipo Dkt. Nchimbi haijawekwa wazi hadharani.
