Mkuu wa Mkoa wa Geita, Alexander Mnyeti ameagiza gari la Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato lipelekwe katika Kituo cha Afya Mganza na kutumika kama gari la Wagonjwa.
Agizo hilo limekuja baada ya Mbunge wa Jimbo la Chato Kaskazini, Cornel Magembe kuomba gari la Wagonjwa la kituo hicho liwekewe tairi baada ya kukaa kwa muda bila kutengenezwa.
Akitoa agizo hilo katika mkutano wa hadhara mbele ya Wananchi wa Kata ya Mganza, Mnyeti amesema ni jambo la aibu na kushangaza kwa Mkurugenzi kushindwa kutoa fedha kwa ajili ya kuweka tairi kwenye gari hilo.
Kutokana na hali hiyo, Mnyeti ameagiza gari analotumia Mkurugenzi lipelekwe katika Kituo cha Afya Mganza na litumike kama gari la Wagonjwa.
