Saudi Arabia Yaomba Msaada Uingereza Baada Ya Kukosa Kwa Marekani

Baba Abby
0

 


Kwa mujibu wa Bloomberg ikinukuu vyanzo vyenye taarifa, serikali ya Saudi Arabia imeiomba Uingereza kutoa msaada wa kijeshi wa moja kwa moja ili kukabiliana na operesheni za Serikali ya Yemen inayoongozwa na Ansarullah, kufuatia hatua ya Marekani kukwepa kujiingiza zaidi vitani.


Hatua hiyo ya Riyadh inakuja wakati ambapo Washington inashikilia mkakati wa Strategic Abstinence, ikiacha ombwe la kiusalama ambalo sasa Saudi Arabia inataka lizibwe na London kupitia ulinzi wa ziada na ushiriki wa kiulinzi.


Ripoti hiyo inaeleza kuwa mashambulizi ya Ansarullah baharini yametekeleza kwa mafanikio mkakati wa A2/AD (Active Denial) kwenye Bahari ya Shamu, jambo lililoongeza shinikizo kwa Riyadh. 


Hata hivyo, wachambuzi wanabainisha kuwa London inasita kuingilia kijeshi kwa hofu ya kupanda kwa bei ya nishati na athari kubwa za kiuchumi.


Kwa upande wake, Serikali ya Yemen inayoongozwa na Ansarullah imesisitiza kuwa taifa lolote litakalojiunga na vita hivyo litakuwa shabaha halali ya kijeshi.

Post a Comment

0 Comments

Post a Comment (0)

#buttons=(Ok, Go it!) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Check Now
Ok, Go it!