Jordan yalaani mashambulizi ya Wahouthi dhidi ya Saudi Arabia

Baba Abby
0

 


Wizara ya Mambo ya Nje na Watu wa Jordan wanaoishi Nje ya Nchi imekemea vikali mashambulizi yanayodaiwa kufanywa na Wahouthi wa Yemen dhidi ya Raia na maeneo ya kiraia nchini Saudi Arabia.


Katika taarifa yake iliyotolewa Jumanne hii Septemba 15, Wizara hiyo ilisema Miji ya Khamis Mushait, Abha na Taif ililengwa kwa makombora ya balistiki na ndege zisizo na rubani.


Jordan imeelezea mashambulizi hayo kama “ukiukaji wa wazi wa mamlaka ya Saudi Arabia”, ikisema pia yanahatarisha usalama, utulivu na uadilifu wa ardhi ya Saudi Arabia.


Wizara hiyo imeongeza kuwa mashambulizi hayo ni “ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa na Mkataba wa Umoja wa Mataifa.”


Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jordan, Balozi Fuad Majali, alieleza mshikamano wa nchi yake na Saudi Arabia, akisema Jordan ina “mshikamano kamili” na Saudi Arabia.


Majali alisema Jordan iko upande wa Riyadh “katika kila hatua inayochukua kulinda usalama wake, utulivu wake, rasilimali zake, pamoja na usalama wa raia na wakazi wake.”

Tags

Post a Comment

0 Comments

Post a Comment (0)

#buttons=(Ok, Go it!) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Check Now
Ok, Go it!