TPSF Na TanTrade Kuimarisha Sekta Binafsi Na Biashara

Baba Abby
0

 



Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), katika jitihada za kuimarisha Sekta Binafsi na kukuza biashara nchini, imefanya mazungumzo na viongozi wa Shirikisho la Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) kwa lengo la kuimarisha ushirikiano katika kuwezesha wafanyabiashara wa Tanzania kushiriki kikamilifu katika biashara za ndani na kimataifa.


Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade, Ephraim B. Mafuru, amesema TanTrade ni kiungo muhimu kati ya Serikali na Sekta Binafsi, hususan katika kukuza na kuendeleza biashara nchini.


Ameeleza kuwa TanTrade iko tayari kuendelea kushirikiana na Sekta Binafsi katika kuwezesha wafanyabiashara wa Tanzania kutumia fursa zilizopo katika masoko ya ndani na nje ya nchi.


Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Bw. Deogratius Massawe, amesema TPSF iko tayari kushirikiana na TanTrade katika kukuza na kuimarisha Sekta Binafsi ili kuongeza ushindani wa wafanyabiashara wa Tanzania katika masoko ya ndani na kimataifa.


Amesema ushirikiano huo utalenga zaidi katika kuwawezesha wafanyabiashara kupata fursa za biashara na uwekezaji, kuboresha mazingira ya biashara nchini, pamoja na kuongeza ushiriki wa Sekta Binafsi katika mikutano, makongamano na majukwaa ya biashara ya kimataifa.


Miongoni mwa maeneo yaliyotiliwa mkazo katika kikao hicho ni pamoja na ushauri kuhusu Sera za Biashara, uimarishaji wa ushiriki wa wafanyabiashara wa Tanzania katika biashara na uwekezaji, tafiti za biashara, pamoja na ushiriki katika mikutano, maonesho na makongamano ya biashara ndani na nje ya nchi.

Tags

Post a Comment

0 Comments

Post a Comment (0)

#buttons=(Ok, Go it!) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Check Now
Ok, Go it!