Zungu amemtetea msanii Dudu Baya dhidi ya madai kwamba amewatapeli Watanzania waliomchangia fedha, akisema michango hiyo haikutokana na faini aliyotozwa na BASATA, bali ilikuwa ni sehemu ya kumuunga mkono katika kampeni yake ya kuhamasisha wanaume “kulinda migongo yao.”
Zungu amesema baadhi ya watu wamekuwa wakidai kuwa Dudu Baya amewatapeli waliomchangia baada ya taarifa kwamba faini yake tayari imelipwa.
“Dudu Baya hatujamchangia kwa sababu ya faini aliyopewa na BASATA, bali tumemchangia kutokana na kile anachokifanya cha kuhamasisha wanaume kulinda migongo. Dudu Baya si kwamba alikuwa hana hiyo pesa, bali sisi Watanzania tulitamani kumchangia muda mrefu sana, hata hivyo yeye hakutaka tumchangie. Tulimuomba kwa mapenzi yetu kwake,” amesema Zungu.
Kauli hiyo imekuja baada ya Suma Mnazareti kumtaka Dudu Baya kuweka wazi kiasi cha fedha alichopokea kupitia michango hiyo na matumizi yake.
