Auliwa Kwa Kukatwa Shingo Na Kutobolewa Macho Arusha

Baba Abby
0

 


Hamis Idd Masimba, mwenye umri wa miaka 24 na dereva wa bodaboda katika Kijiwe cha Mlima CCM, Kata ya Murieti jijini Arusha, ambaye alikuwa ameripotiwa kupotea, amekutwa amefariki dunia katika eneo la Olasiti.


Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa ndugu zake, mwili wa Hamis ulikutwa ukiwa na majeraha makubwa, huku baadhi ya sehemu za mwili zikiwa zimejeruhiwa vibaya.


Ndugu hao wameeleza kuwa baada ya Hamis kupotea, simu yake ilipatikana na mtu aliyedai kuwa ameokota simu hiyo na kuwataka walipie Shilingi 10,000 ili airejeshe. Hata hivyo, muda mfupi baadaye simu hiyo ilizimwa na mawasiliano yakakatika.


Katika juhudi za kumtafuta, ndugu walifika katika eneo walilodhani angeweza kuwa amepita na kukuta viatu vyake, huku pikipiki aliyokuwa akiendesha ikiwa haijapatikana.


Tukio hilo limezua hofu miongoni mwa madereva bodaboda jijini Arusha, huku likifuatia taarifa za matukio mengine ya mauaji yanayowahusisha madereva wa bodaboda katika maeneo mbalimbali.


Kwa sasa, mazingira na sababu za kifo cha Hamis bado hazijathibitishwa rasmi, na uchunguzi wa Jeshi la Polisi unahitajika kubaini kilichotokea pamoja na wahusika wa tukio hilo.

Tags

Post a Comment

0 Comments

Post a Comment (0)

#buttons=(Ok, Go it!) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Check Now
Ok, Go it!